MCHAFUKO WA DAMU NA USAFISHAJI WA DAMU NA MWILI.(DETOX)

KUNA JAMBO LA KIAFYA AMBALO LIMENAWIRI KATIKA JAMII (MITANDAONI, VIJIJINI NA MITAANI) KUHUSU MCHAFUKO NA USAFISHAJI WA MWILI WA BINADAMU KWA KUTUMIA AIDHA MADAWA YA KIENYEJI, VYAKULA AU VINYWAJI.
INAAMINIKA NA WENGI KWAMBA MARA KWA MARA MWILI HUJAA UCHAFU NA HIVYO BASI HUWA INAPASWA KUUSAFISHA ILI KUUNUSURU KUTOKANA NA MARADHI.

HOJA HII INATATANISHA SANA KWA KUWA MWILI WA BINADAMU UNA VIUNGO VYAKE AMBAVYO KAZI YAKE NI KUSAFISHA MWILI KILA SEKUNDE BILA HATA MTU KUJUWA.
SWALI LETU KUBWA LA LEO NI:
JE, MCHAFUKO WA DAMU NI NINI?
NA JE, HUKU KUSAFISHA DAMU NA MWILI KUNA MANUFAA GANI?

MCHAFUKO WA DAMU NI NINI?

NENO HILI LINA MAANA NYINGI KULINGANA NA ANAYELITUMIA NA KULINGANA NA MUKTADHA NA WAKATI MWINGINE HUWAPOTOSHA WANA JAMII.

KWA KIZUNGU NENO HILI LINAAMBATA NA MANENO KAMA VILE DETOX, DETOXIFICATION, SEPSIS, SEPTICEMIA, UREMIA, HYPERBILIRUBINEMIA NK. MANENO HAYA YANA MAANA TOFAUTI KABISA IKILINGANISHWA NA MATUMIZI YA NENO HILI HAPA KWETU.

BAADHI YA MAANA ZAKE NI:
Kuwepo kwa vidudu kwenye damu yaani SEPTICEMIA. Vidudu hivi ni kama vile bakteria, virusi, fangi au protozoa.
 Kuongezeka kwa uchafu unaotokana na viungo vya mwili kushindwa kufanya kazi
 Kiwango cha juu cha masalio na chembechembe au uchafu unaotokana na:
Usagaji wa chakula kwenye tumbo, au
Madawa ikiwemo sumu na mihadarati au
Miali yaani radiations kwenye nyanja za matibabu nk

FAHAMU KWAMBA…
Mwili una uwezo wake wa kibinafsi wa kusafisha mazingara yake ya ndani kama vile damu, pafu, figo, ini, matumbo, ubongo, wengu nk bila hata wewe kuwa na ufahamu wa matukio haya isipokuwa wakati viungo vimedhoofika kama vile ugonjwa wa figo au viungo vinginevyo ambapo usaidizi huhitajika.

NDANI YA ULINGO WA MATIBABU NA AFYA, MCHAFUKO WA DAMU ILE HALI YA Kuwepo kwa vidudu kwenye damu yaani SEPTICEMIA. Vidudu hivi ni kama vile bakteria, virusi, fangi au protozoa

KUSAFISHA DAMU NA MWILI KUNAAMBATANA NA HALI FULANI ZA KIAFYA.

  • UGONJWA WA FIGO DIALYSIS
  • MIHADARATI NA ULEVI WA POMBE NA MADAWA YA KULEVYA
  • UGONJWA WA MANJANO/INI
  • ACIDOSIS/ALKALOSIS (BICARBONATE ETC)
  • TUMOR LYSIS SYNDROME
  • DECOMPRESSION SICKNESS

MBINU ZA KUSAFISHA DAMU ZINAZOENEZWA

  • DAWA ZA MIZIZI
  • CHAI ZA MADAWA YA KIENYEJI
  • MCHANGANYIKO WA SHARUBATI/JUICE ZA MABOGA
  • MIZIZI
  • TANGAWIZI/MDALASINI/ NA VIUNGO VYENGINE
  • MALIMAU NA MATUNDA MENGINEO
  • MFUNGO MKAVU
  • MFUNGO WA MAJI
  • MFUNGO WA MATUNDA
  • MFUNGO WA MADAWA